Mashindano ya shule za sekondari Afrika Mashariki yaanza Uganda

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya mwaka huu ya michezo ya shule za upili ukanda wa Afrika Mashariki yameanza rasmi siku ya Jumapili katika shule ya Bukedea nchini Uganda.

Mashahindano hayo ya wiki moja yanaandaliwa  atika wilaya ya Bukedea na yalifunguliwa Jumamosi.

Kwa upande  wa wavula, wawakilishi wa Kenya St. Joseph Boys Kitale na Highway Secondary zimejumuishwa kundi A pamoja na St Mary’s Kitende na Bukedea Comprehensive zote za Uganda, hali kadhalika Benjamin Mkappa ya Tanzania.

Kundi B linasheheni St Julian na Amus College zote za Uganda na Appe Rugunga ya Rwanda, Musingu High ya Kenya na Kalangalala kutoka Tanzania.

Soka ya wasichana kundi A lina Nyakach Girls na St. Joseph’s kutoka Kenya, St. Noah na Kawempe Muslim za Uganda na GS Remera Rukoma Kamonyi ya Rwanda.

Butere Girls wa Kenya wamerushwa kundi B pamoja na Tanzanite Secondary, Alliance ya Tanzania na Rines na Amus College zote za Uganda.

Kenya pia inashiriki mpira wa mikono, raga ya wanaume saba na 15  upande, mpira wa wavu, mpira kikapu na mpira wa pete.

Share This Article