Makundi ya FEASSSA yatajwa

Marion Bosire
2 Min Read

Shirikisho la michezo baina ya shule za upili kanda ya Afrika Mashariki( FEASSSA), limetaja makundi ya timu zitakazoshiriki michezo ya mwaka huu itakayoandaliwa mjini Mbale nchini Uganda.a

Mashindano hayo yatakayoshirikisha michezo ya soka, raga, vikapu, tenisi, voliboli, netiboli, mbio, uogeleaji miongoni mwa zingine,yanatarajiwa kung’oa nanga tarehe 16 hadi 28 mwezi huu.

Hapo jana, shirikisho hilo lilitaja makundi na mpangilio wa kipute kama ifuatavyo: katika soka ya wavulana, kundi A litajumuisha Highway secondary na St.Joseph za Kenya, Bukedea Comprehensive na St.Mary’s Kitende za Uganda na Benjamin Mkapa ya Tanzania.

Kundi B linajumuisha Amus College na St. Julian za Uganda, Musingu High – Kenya, Kalangalala Secondary – Tanzania na Ape Rugunga – Rwanda.

Kwenye raga ya wachezaji 15 kila upande, All Saints na Lenana za Kenya zimo kwenye kundi A pamoja na St. Mary’s Kisubi na Namilyango College za Uganda, huku Butula Boys na Kitondo za Kenya zikipangiwa kukabana na Kings College Budo na Makerere College za Uganda.

Raga ya wachezaji saba kila upande inajumuisha Bwake Boys, Vihiga High, St. Mary’s Yala na Kisii (zote za Kenya), Jinja SS, Kiira College, Dr. Obote College (zote za Uganda) na timu moja ya Rwanda.

Upande wa akina dada tunazo Kinale SS, St. Joseph’s, St. Theresa’s, Nyagicheche (zote za Kenya), Nkoma SS, Jinja SS, PMM Girls, Kijjabwemi (zote za Uganda) na moja ya Rwanda.

Tenisi ya meza ya wavulana inajumuisha Mbogo mixed, Mbogo College, Seroma Christian, Kibuli SS ( zote za Uganda) na St. joseph ya Kenya. Ya wasichana inajumuisha Mbogo College, Mbogo High, Kibuli SS, Mbogo Mixed (zote za Uganda) na Kesogon ya Kenya.

TAGGED:
Share This Article