Hellen Obiri alinyakua nishani ya shaba katika mbio za marathoni ya wanawake katika siku ya mwisho ya michezo ya Olimpiki mapema Jumapili jijini Paris, Ufaransa.
Obiri aiyekuwa askishiriki marathoni ya Olimpikki kwa mara ya kwanza alikuwa katika kundi la uongozi kabla ya kuzidiwa maarifa katika mita 200 za mwisho na kuridhia nishani ya shaba kwa saa 2 dakika 23 na sekunde 10.
Sharon Lokedi ambaye pia alikuwa ashiriki Olimpiki kwa mara ya kwanza alimaliza wa nne huku bingwa mtetezi Peres Jepchirchir akiambulia nafasi ya 15.
Sifan Hassan wa Uholanzi alishinda dhahabu kwa saa 2 dakika 22 na sekunde 53 akifuatwa na Tigst Assefa wa Ethiopia aliyenyakua fedha.
Ilikuwa medali ya tatu kwa Sifan baada ya kunyakua shaba za mita 5,000 na 10,000.
Kenya imeibuka taifa bora Afrika kwa medali 4 za dhahabu, fedha 2 na shaba 5 ikifuatwa na Algeria kwa dhahabu 2 na shaba moja, huku Afrika Kusini wakihitimisha nafasi tatu bora kwa dhahabu 1 fedha 3 na shaba 2.