Walanguzi wa mihadarati wanaswa Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Walanguzi wa mihadarati wanaswa katika uwanja wa ndege wa JKIA.

Maafisa wa polisi wa kukabiliana na mihadarati katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wamemnasa mlanguzi wa dawa za kulevya, akisafirisha gramu 1,080 za Cocaine.

Mshukiwa huyo Bioma Alice Gbassay kutoka Sierra Leone, aliwasili katika uwanja huo wa ndege akiwa safarini kuelekea Mumbai, kabla ya maafisa wa uhamiaji kuchukua mizigo yake na kuupeleka katika afisi za maafisa wa kukabiliana na dawa za kulevya.

Kulingana na idara ya upelelezi wa maswala ya jinai DCI, baada ya mzigo wake kufanyiwa upekuzi, mihadarati hiyo ilipatikana ikiwa imefichwa katika sehemu mbali mbali ya mizigo yake.

Bidhaa zilizosingiziwa kuwa sabuni pia zilipatikana, na baada ya uchunguzi wa maabara zilibainishwa kuwa dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Wakati huohuo, maafisa wa polisi pia walimkamata mwanaume aliyekuwa akisafirisha bangi kutoka Malaba kuelekea Jijini Nairobi.

Emmanuel Erony alipatikana na vipande vikubwa 19 vya bangi vyote vya gramu 19,810 vya dhamani ya shilingi 990,500.

washukiwa hao wawili wanasubiri kufikishwa mahakamani.

TAGGED:
Share This Article