Watatu kwenye kinyang’anyiro cha Inspekta Mkuu wa Polisi

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa watatu wanawania kiti cha Inspekta Mkuu wa Polisi kumrithi Japhet Koome aliyejiuzulu wiki iliyopita.

Watatu hao ni pamoja na kaimu Inspekta Mkuu Douglas Kanja,Kamanda wa chuo cha mafunzo ya Polisi Nyale Munga na Kamanda wa Akademia ya jeshi Aphaxard Kiugu.

Majina hayo matatu yatawasilishwa bungeni na Rais William Ruto, huku kila mmoja akihojiwa na kamati ya Bunge, kabla ya kurejesha majina  kwa Rais kwa uteuzi rasmi.

Tayari mashirika mbalimbali ya kijamii yamejitokeza kutaka mabadiliko ya uteuzi ya Inspekta Mkuu  na kurejesha mfumo wa zamani, ambapo tume ya polisi ilijukumiwa na uteuzi huo kinyume na ilivyo kwa sasa ambapo ni Rais anayefanya uteuzi.

Website |  + posts
Share This Article