Euro 2024: Uhispania yawatimua wenyeji Ujerumani

Tom Mathinji
1 Min Read

Waandalizi wa makala ya 17 ya bara Ulaya Ujerumani, wameondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kulazwa magoli mawili kwa moja na Uhispania katika robo fainali.

Mabao ya Uhispania yalitingwa kupitia wachezaji wa akiba Dani Olmo na Mikel Merino namo dakika za 51 na 119 mtawalia nalo la Ujerumani likafungwa na mchezaji wa akiba Florian Wirtz dakika ya 89.

Mchuano huo uliisha na kadi moja nyekundu, aliyoonyeshwa beki matata wa Uhispania na klabu ya Real Madrid Dani Carvajal alipomwangusha Musiala.

Hii ni mara ya kwanza kwa Uhispania kuwabandua waandalizi wa mashindano ya aina yeyote.

Kwenye robo fainali ya pili, Ufaransa ilifuzu kwenye nusu fainali kwa kuilaza Ureno Kwa matuta 5-3 kufuatia sare ya yai.

Washindi hao watachuana katika nusu fainali ya tarehe tisa saa nne usiku.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *