Wanaume wawili wamefikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya Milimani Rose Ndubi, kwa kosa la kutumia lugha ya dharau kwa mjumbe wa Kikuyu Kimani Ichungw’ah na waziri wa fedha Njuguna Ngung’u.
Inadaiwa kuwa mshtakiwa kelvin Wafula alitumia mtandao wa WhatsApp kutuma ujumbe wa kutishia kumuua waziri wa Hazina kuu.
Mshtakiwa wa pili Stephen Kamau alituma ujumbe wa kutishia kumwangamiza kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Ichunng’wa.
Hata hivyo, wawili hao kupitia kwa wakili wao, walikana mashtaka hayo na kuomba mahakama kuwaachilia kwa dhamana ndogo kutokana na hali yao ya maisha.
Mahakama iliridhia ombi hilo na kuwaachilia kwa dhamana ya shilingi 100,000 kila mmoja.
Tukio hilo linajiri kufutia maandamano ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka huu na kundi la vijana wa Gen Z, ambayo yalisababisha vifo na majeruhi wengi kote nchini.