Msemaji wa ikulu ya rais Hussein Mohamed ametangaza kwamba rais William Ruto amebuni kundi la kushughulikia malalamishi yote yaliyoibuiliwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta.
Kupitia akaunti yake ya mtandao wa X, Hussein alifafanua kwamba kundi hilo litaongozwa na mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei.
Haya yanajiri baada ya kiongozi wa nchi kujadiliana na mtangulizi wake kuhusu ufadhili wa mipango ya afisi ya rais wa nne wa jamhuri ya Kenya.
Mkuu wa mawasiliano wa afisi ya rais wa nne wa Kenya Kanze Dena alifanya mkutano na wanahabari awali ambapo alielezea kwamba serikali haijakuwa ikitoa pesa hizo inavyohitajika kisheria.
Dena alisema kwamba rais Kenyatta ndiye amekuwa akifadhili mipango ya afisi yake na kwamba afisi hiyo imepokea shilingi milioni 28 pekee kati ya milioni 655 ilizotengewa kwenye bajeti ya mwaka 2022/2023.
Sheria kuhusu mafao ya rais mstaafu imeelezea baya kuhusu mafao kwa rais mstaafu yakiwemo malipo ya takrima kila mwezi, pesa za burudani, pesa za kugharamia makazi, afisi stahiki, magari mawili mapya yatakayobadilishwa kila baada ya miaka miwili na pesa za matumizi kwenye afisi yake.