Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 itachuana na Burundi Jumapili jioni, katika mkumbo wa kwanza raundi ya nne kufuzu kwa Kombe la Dunia .
Mechi hiyo itakasakatwa katika uchanjaa wa Abeba Bikila mjini Adis Ababa,Ethiopia, huku marudio yaliandaliwa nchini Kenya wikendi ijayo.
Kenya iliyowasili Ethiopia juzi ilifanya mazoezi ya mwisho Jumamosi jioni kujiandaa kwa pambano hilo.
Mshindi wa jumla baadaya mikondo miwili atafuzu kushiriki fainali za kombe la Dunia zitakazoandaliwa Novemba mwaka huu katika Jamhuri ya Dominika.