Mikakati yawekwa kuimarisha afya ya mdomo

Kevin Karunjira
1 Min Read

Katibu katika Idara ya Huduma za Hatibabu Harry Kimtai amefanya mkutano wa kimkakati na Timu ya Afrika Mashariki ya Colgate-Palmolive ili kuimarisha huduma za afya ya mdomo kote nchini.

Majadiliano hayo yalilenga kuendeleza mpango wa afya ya mdomo kwa wanafunzi katika shule mbalimbali. Aidha, mpango huo unalenga kukuza mazoea mazuri ya usafi wa mdomo miongoni mwa watoto.

Wakati wa mkutano huo, pande zote mbili ziliazimia kutoa mafunzo kwa wauguzi na wahudumu wa afya ya jamii katika kaunti mbalimbali.

Mpango huu unalenga kuimarisha elimu ya afya ya mdomo kwa jamii na kuhakikisha kuwa inawafikia watu ambao hawajapata huduma hizo ipasavyo.

Kimtai alisisitiza dhamira ya Wizara ya Afya  kuafikia upatikanaji sawa wa huduma bora za afya ya mdomo kwa Wakenya wote.

Ushirikiano huu unaashiria nguzo muhimu katika kukuza utamaduni wa usafi wa mdomo, hatua itakayoboresha matokeo ya afya ya mdomo kote nchini Kenya.

TAGGED:
Share This Article