KCB watinga fainali ya kombe la Mozzart huku nusu fainali kati ya Police FC na Leopards ikitubuka

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya Commercial Bank wamejikatia tiketi kwa fainali ya kombe la Mozzart bet baada ya kuwalemea Kariobangi Sharks magoli 4-2, kupitia matuta ya penati kufuatia sare ya bao moja baada ya dakika 120 katika uwanja wa Police Sacco Jumapili Adhuhuri.

Derrick Otanga alipachika bao kwanza kwa KCB  kunako dakika ya 77, kabla ya Fortune Omotto kusawazishia Sharks dakika mbili baadaye.

Hata hivyo nusu fainali ya pili kati  ya AFC Leopards  na Police FC ilitibuka kunako dakika ya 60, baada ya mashabiki wa Ingwe kumvamia na kumjeruhi refarii .

Police walikuwa kifua mbele goli 1 kwa sifuri kufikia wakati wa kutibuka kwa mchuano huo.

Semi fainali hiyo itakamilika Jumatatu kwa dakika 30 za mwisho.

Mshindi atakumbana na KCB katika fainali ya mwezi ujao, huku mshindi akituzwa kombe shilingi milioni 2 na tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika.

 

Share This Article