Mamia ya wasafiri wataabika kufuatia mgomo wa matatu

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamia ya Wakenya walikwama baada ya kukosa usafiri kufuatia mgomo wa wahudumu wa matatu ulioanza katika maeneo mbalimbali kote nchini mapema leo Jumatano.

Katika baadhi ya maeneo, makanga waliwafurusha wahudumu wachache wa matatu waliokuwa tayari kazini na kuwalazimu kuondoka.

Wenye matatu wanapinga agizo la serikali kutaka kuwakagua upya kuhusu uweledi wao wa kuendesha magari.

Baadhi ya kaunti ambazo zimeathirikika pakubwa na mgomo huo ni Nyeri, Bomet, Nyandarua, Kericho, Nakuru na Mombasa.

Mgomo huo umewaacha abiria wakihangaika wasijue la kufanya.

Wenye magari wanagoma kupinga pendekezo la Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen kutangaza madereva kufanyiwa tathmini mpya ili kubaini ufaafu wao.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *