Serikali ya kitaifa itakamilisha miradi ya barabara katika kaunti ya kwale kwa wakati unaofaa.
Haya ni kwa mujibu wa kiongozi walio wengi katika bunge la kitaifa kimani Inchungwa aliyekua akizungumza katika halfa ya kuchangisha pesa kusaidia chama cha ushirika kiitwacho “Tuchapekazi LungaLunga Subcounty Sacco” huko Kwale ambapo jumla ya shilingi milioni 3.3 zilikusanywa.
Inchungwa alisema kwamba ujenzi wa barabara ya kutoka Kwale kuelekea kinango pamoja na ujenzi wa daraja la funzi huko Msambweni umekwama kwa sababu ya ukosefu wa fedha.
Hata hivyo aliahidi kwamba barabara ya miradi hiyo miwili itakamilika kabla ya mwisho wa muhula wa kwanza wa Rais William Ruto.
Daraja la Mwachande huko LungaLunga lililosombwa na mafuriko ya mwaka 1997 limetengewa jumla ya shilingi milioni 153 kwa awamu ya kwanza na pili na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi julai mwaka huu.
Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya kwale Fatuma Achani alisema kwamba kuboreshwa kwa miundo msingi ya barabara katika Kaunti ya kwale kutaimarisha sekta ya uchukuzi na biashara katika ukanda wa kusini mwa pwani.