Waakilishi wa Kenya katika mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa wanawake nchini Misri,katika mpira wa wavu Kenya Prisons na Kenya Commercial Bank wamejikatia tiketi kwa robo fainali.
Prisons wametinga kwota fainali kufuatia ushindi wa seti tatu kwa bila dhidi ya Customs ya Nigeria za 25-10, 25-18 na 25-13, wakati KCB ikiwazidia maarifa ASEC ya Ivory Coast seti tatu bila za 25-6, 25-18 na 25-13.