Rais William Ruto anaongoza mkutano wa mataifa manne wanachama wa shirika la IGAD, kuhusu mchakato wa amani nchini Sudan Jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Mkutano huo unajumuisha waakilishi kutoka Sudan kusini, Ethiopia na Djibouti.
Kwenye taarifa, msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, alisema mkutano huo unalenga kuboresha ushirikiano miongoni mwa wanachama na kuhakikisha amani na udhabiti zinadumu nchini Sudan.
Hussein alisema kuwa kinachotiliwa mkazo ni kukomeshwa kwa uhasama, kurahihisha usambazaji wa misaada ya kibinadamu na kuchukua hatua madhubuti za kuleta amani ya kudumu nchini Sudan.
Mkutano huo pia unalenga kubuni mfumo endelevu ambao utachangia maridhiano na ustawi nchini Sudan.