Kongamano la kimataifa la uwekezaji kuanza Jumanne Kakamega

Boniface Musotsi
1 Min Read

Kongamano la kimataifa la uwekezaji linatarajiwa kuanza Jumanne katika Chuo Kikuu cha Masinde Muliro, kaunti ya Kakamega.

Kongamano hilo litakalokamilika tarehe 22 mwezi huu linawaleta pamoja zaidi ya washiriki 2,000.

Litafunguliwa rasmi na Rais William Ruto.

Kikao hicho pia kitahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Biashara barani Afrika(KCIDA) Wamkele Mene na balozi wa Marekani humu nchini Margaret Whitman.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa UweKezaji na Maendeleo Elizabeth Asichi, kaunti ya Kakamega itatumia fursa hiyo kupata wawekezaji wanaotarajiwa kupiga jeki miradi mbalimbali ya kaunti hiyo kama vile kukamilishwa kwa hospitali ya rufaa na mafunzo ya Kakamega iliyo na vitanda 750.

Boniface Musotsi
+ posts
Share This Article