Chui yalenga ushindi wa 6 mtawalia Bukhungu

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya AFC Leopards itashuka uwanjani Bukhungu Kakamega jumapili dhidi ya wenyeji Kakamega Homeboyz, katika derby  maarufu kama “ingo derby” .

Ngarambe hiyo itang’oa nanga saa tisa alasiri huku halaiki ya mashabiki ikitarajiwa kuhudhuria.

AFC leopards ukipenda Ingwe, wameandikisha  musururu wa matokeo mazuri katika mechi tano zilizopita ya hivi karibuni ikiwa dhidi ya Muranga Seal,waliposhinda  bao moja.

Ushindi huo wa tano uliipandisha timu hiyo hadi nafasi ya nane ligini.

Katika mechi ya awamu ya kwanza msimu huu  Disemba 17  mwaka jana , chui alimngata Homeboys magoli mawili kwa sufuri na sasa Jumapili huenda  ikawa mechi ya kulipiza  kisasi kwa Homeboyz .

Hata hivyo Kakamega , ambao pia ni washindi wa kombe la Mozzart Bet, wameandikisha matokeo chanya katika mechi tano zilizopita wakitoka  sare mbili, kupoteza mara mbili na ushindi mmoja .

Share This Article