Wakulima wa kahawa kufurahia malipo bora

Martin Mwanje
1 Min Read
Wakulima wa kahawa nchini wanatazamiwa kufurahia mavuno ya walichopanda baada ya kubainika kuwa watakuwa wanapokea shillingi 80 kwa kila kilo ya zao hilo. 
Hii ni kwa mujibu wa katibu wa vyama vya ushirika nchini Patrick Kilemi aliyeyazungumza haya akiwa katika hafla ya hamasisho la wakulima wa kahawa eneo bunge la Kabuchai, kaunti ya Bungoma.
Viongozi wa kaunti ya Bungoma wakiongozwa na Gavana Kenneth Lusaka na Seneta wa kaunti hiyo Wafula Wakoli wamevitaka vyama vya ushirika kukoma hulka ya kulipa wakulima pesa taslimu ili kukabili wizi wa fedha ambao umekuwa ukishuhudiwa mara kwa mara.
Hata hivyo, wamesisitiza haja ya kuwepo kwa usawa kwa wakulima nchini, wakisema kuwa serikali imekuwa ikiegemea wakulima wa maeneo fulani nchini huku wengine wakitelekezwa.
Share This Article