Arsenal wapigwa kumbo nyumbani na West Ham

Dismas Otuke
1 Min Read

Majuma kadhaa baada ya kuibandua Arsenal katika kombe la Carabao, West Ham United ilidhihirisha ubabe wake ilipokosa adabu na kuititiga The Gunners mabao 2 -1 katika mechi ya ligi kuu ugani Emirates Alhamisi usiku.

Tomas Soucek alifungua ukurasa kwa goli la kwanza dakika ya 13 kwa washika nyundo akiunganisha pasi ya James Bowen, kabla ya Konstantinos Mavropanos kutanua uongozi wa West Ham dakika ya 55 akiunganisha krosi ya James Wardprowse.

Arsenal wanasalia alama 2 nyuma ya viongozi Liverpool katika jedwali la EPL.

Share This Article