Chama cha UDA kimeahirisha uchaguzi wake wa mashinani

Tom Mathinji
1 Min Read

Chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA), kimeahirisha uchaguzi wake wa mashinani ambao ulikuwa ufanyike tarehe tisa mwezi Disemba mwaka 2023.

Kupitia kwa taarifa, katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala, alisema uchaguzi huo sasa utaandaliwa mwezi Aprili mwaka 2024.

Kulingana na Malala, zoezi hilo limeahirishwa kufuatia mkutano wa baraza la kitaifa la chama hicho lilioandaliwa tarehe 18 mwezi Novemba mwaka 2023, ulioongozwa na kiongozi wa chama hicho Rais William Ruto.

Alidokeza kuwa uchaguzi huo utaandaliwa katika awamu tatu, tarehe 12, 19 na tarehe 26 mwezi Aprili mwaka 2024.

“Tunawahimiza wawaniaji kuendelea kujisajili, huku usajili ukiwa wazi hadi tarehe 22 mwezi Machi mwaka 2024 saa kumi na mbili jioni,” alisema Malala.

Share This Article