Uhispania watwaa kombe la UEFA Nations League

Dismas Otuke
1 Min Read

Uhispania ilinyakua kombe la ligi ya mataifa ya Ulaya baada ya kuilemea Croatia mabao 5-4 kupitia matuta ya penalti kufuatia sare tasa katika dakika 120.

Fainali hiyo ilipigwa Jumapili usiku uwanjani Roterderm, Uholanzi ikiwa mara ya kwanza kwa Uhispania kushinda kombe hilo.

Timu zote zilicheza kwa tahadhari kubwa huku zikibuni nafasi haba za kufunga mabao.

Katika penalti, timu zote ziliunganisha penalti 4 huku zikikosa moja na hatimaye kipa wa Uhispania Unai Simon akapangua penalti ya Bruno Petkovic kabla ya Dani Carvajal kuunganisha mkwaju wa ushindi.

Lilikuwa kombe la kwanza kwa Uhispania tangu washinde kombe la Euro mwaka 2012 huku Croatia wakipoteza fainali ya pili tangu washindwe na Ufaransa kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2018.

Italia ilimaliza ya tatu baada ya kuwashinda wenyeji Uholanzi mabao 3-2.

Website |  + posts
Share This Article