37 wafariki kwenye mpango wa usajili wa wanajeshi Congo Brazzaville

Marion Bosire
1 Min Read

Vijana 37 wameripotiwa kufariki kufuatia mkanyagano uliotokea katika uwanja mmoja wa michezo jijini Brazzaville nchini Congo.

Kulingana na ripoti rasmi, mkasa huo ulitokea usiku wa Jumatatu Novemba 20, 2023, katika uwanja wa michezo wa Ornano ambapo watu walifariki na wengine kujeruhiwa.

Vifo 37 viliripotiwa huku watu wengine kadhaa wakiachwa na majeraha kulingana na ripoti ya jopo la dharura linaloongozwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Anatole Collinet Makosso.

Share This Article