Kuna haja ya tani 2,000 za oksijeni kuzalishwa chini ya kiwanda kipya cha oksijeni kilichozinduliwa katika kaunti ya Kilifi.
Kiwanda hicho kilizinduliwa ili kuziba pengo kwa theluthi moja kwani tani 7000 za oksijeni zinahitajika Afrika Mashariki.
Uzinduzi huo uliowekezwa shilingi bilioni 2.8 na mataifa ya Canada na Japani unalenga kutoa oksijeni kwa maelfu ya watu siyo tu Afrika Mashariki bali barani Afrika.
Shirika la Afya Duniani, WHO linakadiria kuwa wagonjwa 500,000 duniani wanakumbwa na uhaba wa oksijeni kila siku huku nchi nyingi zikitatizika kutoa huduma hiyo.
Humu nchini pekee, maelfu ya wagonjwa wanakabiliwa na matatizo ya kutishia maisha na hivyo miundombinu bora inahitajika ya kuweza kupunguza uhaba huo wa uzalishaji wa gesi hiyo muhimu.
Magavana Gideon Mungaro (Kilifi) na Abdulswamad Shariff (Mombasa) wameahidi kupiga jeki mradi huo wa kuzalish gesi ya okisjeni ili kusaidia wagonjwa wenye mahitaji ya bidhaa hiyo hospitalini.