Kampuni ya maji ya Nyahururu “NYAHUWASCO” imekuwa ikiandikisha hasara kupitia kwa mianya iliyopo ya kiufundi na vitendo vya kihasidi kama wizi wa maji.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi ww afisi mpya za NYAHUWASCO mjini Nyahururu, mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bernard Mbugua alilalamika kwamba kampuni inakumbwa na matatizo kwa sababu wanakusanya pesa kidogo.
Mbugua alionya watendakazi wa kampuni hiyo kuhusu hali ya kupotea kwa pesa akiwataka waisuluhishe haraka iwezekanavyo na akahimiza Kila mmoja kuwajibika kazini.
Gavana Joshua Irungu aliunga mkono matamshi ya mkurugenzi mtendaji akisema huenda wakalazimika kuongeza ada za maji iwapo mianya iliyopo haitazibwa.
Alisema visa vya wizi wa maji vimeongezeka mno katika eneo la Marmanet ambapo wakazi wengi wanatumia maji waliyounganishiwa kinyume cha sheria.