Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesema hatakubali tishio lolote kwa taifa la Somalia kufuatia hatua ya Ethiopia ya kusema kwamba huenda ikatambua Somaliland kama taifa huru.
Somaliland ni eneo lililojitenga ambalo halitambuliwi kama nchi huru ulimwenguni na ni himaya ya Somalia.
Ilidai kuwa huru kwenye mapatano na Ethiopia kuhusu kufikia bandari.
Matamshi makali ya Rais Sisi ni ishara kwamba Misri huenda ikahusika kwenye mzozo ambao umeibua wasiwasi upya katika eneo la upembe wa Afrika.
Somaliland ilijitangaza kuwa taifa huru kutoka kwa Somalia mwaka 1991 na mapatano kati yake na Ethiopia kuhusu bandari bado hayajakamilishwa.
Mapatano hayo ambayo yameikera Somalia huenda yakawa jambo zuri kwa Ethiopia iwapo yatakamilishwa kwa sababu haina bandari.
Rais Sisi alikuwa akizungumza kwenye mkutano na wanahabari akiwa na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud aliyemzuru.
Januari mosi, 2024, mapatano kati ya Ethiopia na Somaliland yalitangazwa ambayo yalisema kwamba Ethiopia itatambua eneo hilo kuwa huru na kujaribu kushinikiza utambuzi kimataifa kwa kubadilishana na eneo la bandari.
Ethiopia hutumia bandari ya Djibouti.