10 wakamatwa kufuatia shambulizi dhidi ya kituo cha polisi Kakamega

Martin Mwanje
1 Min Read
Washukiwa wa uhalifu waliokamatwa na maafisa wa upelelezi Kakamega

Watu 10 wamekamatwa kuhusiana na shambulizi lililotekelezwa siku chache zilizopita dhidi ya kituo cha polisi cha Emakale katika kaunti ndogo ya Matungu, kaunti ya Kakamega. 

10 hao walikamatwa katika operesheni ya pamoja iliyoongozwa na OCS wa kituo cha polisi cha Matungu kwa kushirikiana na maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI.

Maafisa wa usalama wanasema wameimarisha uchunguzi kuhusiana na shambulizi hilo lililosababisha kuharibiwa kwa nyaraka za umma na mali ya afisa mmoja wa polisi.

Washukiwa waliokamatwa kwa sasa wanazuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani.

 

 

Website |  + posts
Share This Article