Zulia mpya kukitwa Uwanjani Nyayo, kabla ya Kip Keino Classic

Korir amefichua kuwa Wizara ya Michezo imeidhinisha na kuanza mchakato wa kununua zulia mpya inayotarajiwa kukitwa katika kipindi cha majuma mawili yajayo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waandalizi wa makala ya sita ya mashindano ya kimataifa ya Kip Keino Classic Continental Tour, wametangaza kuwa serikali itaondoa zulia iliyo katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo na kukita nyingine mpya, kabla ya mashindano ya mwaka huu tarehe 31 mwezi ujao.

Zulia ya saa uwanjani nyayo imechakaa na haiko katika hali ya kutumika kuandaa mashindano ya kimataifa.

Mkurugenzi wa mashindano hayo Barnaba Korir, amesema wanatarajia kuandaa mashindano bora zaidi kuliko makala matano yaliyopita, huku wakiwaalika wanariadha bora duniani wa mbio fupi fupi.

Korir amefichua kuwa Wizara ya Michezo imeidhinisha na kuanza mchakato wa kununua zulia mpya inayotarajiwa kukitwa katika kipindi cha majuma mawili yajayo.

Mkondo wa kwanza wa mashindano ya Continental Tour uliandaliwa tarehe 29 mwezi jana na utafuatwa na ule wa Botswana Grand Prix leo, kabla ya msururu wa Tokyo, Japan, tarehe 18 mwezi ujao.

Mkondo wa nne utafanyika baina ya Mei 22 na 24 mjini Zagreb, ukifuatwa na ule wa Poland Mei 30.

Website |  + posts
Share This Article