Zuchu atuma watangazaji wa Wasafi kwa Diamond, ataka kuolewa

Zuchu anahisi kwamba uchumba wa miaka minne umekuwa sugu, anataka ndoa sasa.

Marion Bosire
2 Min Read

Mwimbaji wa Tanzania Zuhura Othman maarufu kama Zuchu, amewatuma watangazaji wa kipindi cha Mashamsham cha Wasafi Fm kwa mkubwa wao Diamond Platnumz ambaye ni mpenzi wake.

Akihojiwa kwenye kipindi hicho jana, Zuchu aliwataka watangazaji hao wakamwambie Diamond amwoe kwani uchumba wao wa zaidi ya miaka minne umegeuka na kuwa kile alichokitaka kuwa uchumba sugu.

Kuhusu matukio kwenye uhusiano wao wa kimapenzi, Zuchu ambaye aliwahi kutangaza kwamba ameachana na Diamond alisema yamekuwa mengi tu.

Alianza kwa kusifia Diamond akisema, “Kwanza mimi kwa mpenzi wangu kwanza nimpe maua yake.” kisha akendelea kuelezea kwamba anahisi kwa wapenzi wote wa awali wa Diamond yeye ndiye amepitia njia nyepesi.

“Unajua mapenzi bwana yana vitu vingi na unajua wanaume, Ah! wanaume wako kama watoto wachanga.” alielezea binti huyo wa Khadija Kopa akisema huwa anajirudia sana anapomkosoa Diamond.

Lakini kati ya matukio yote lililomkera zaidi ni hatua ya Diamond ya kumpiga busu mwanamuziki wa Ghana Fantana kwenye kipindi cha Netflix cha Young, Famous & African.

Zuchu alisema alifahamu hilo kupitia mitandao ya kijamii kisha akafungulia kwenye runinga kujionea akiwa nyumbani kwa Diamond akimpangia chumba.

Diamond wakati huo alikuwa ameitwa Ikulu na Rais Samia Suluhu na Zuchu anasema kama angekuwa karibu hajui angemfanyaje.

Mwimbaji huyo hata hivyo anakiri kuwapigia simu nyingi wote waliokuwa wamempeleka Diamond Ikulu ambao hawakuchukua simu zake lakini baadaye alitulia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *