Zoezi la ukusanyaji saini kumbandua rais Ruto ni mbwembwe tu, asema Gachagua

Francis Ngala
1 Min Read
Naibu rais Rigathi Gachagua: Photo - Twitter

Naibu rais Rigathi Gachagua ametaja hatua ya kinara wa upinzani Raila Odinga ya kutaka kumng’atua rais William Ruto mamlakani kutumia ukusanyaji wa saini kutoka kwa wakenya kama wazo bonzo na ambalo halina mwelekeo wowote.

“Wanasema watamwondoa Ruto mamlakani. watafanyaje hivyo iwapo walishindwa kumtoa wakati hakuwa mamlakani? Gachagua alisema kwa mshangao, huku akisisitiza kwamba katiba ya taifa hili halina kifungu kinachoelekeza ukusanyaji wa sahihi ili kubandua rais aliye mamlakani.

Akiongea hii leo katika hafla ya mazishi eneo bunge la Mathira, Gachagua amesema uchaguzi hauamuliwi kwa saini huku akiwasihi viongozi wa upinzani kukubali matokeo ya uchaguzi yaliodhihirisha ushindi wa William Ruto.

“Hata wakikusanya sahihi milioni 10, watazipeleka wapi na kwa nani ? Maswala ya uchaguzi hayaamuliwi kwa saini yanaamuliwa kwa Kura na kuna siku rasmi ambayo ilitengwa kwa shughuli hiyo.” alisema Rigathi Gachagua.

Wakati huo huo naibu rais amewarai wakenya kuendelea kujikakamua katika juhudi zao kwani makelele ya Azimio hayababaishi serikali.

Kinara wa Azimio Raila Odinga katika uwanja wa Kamkunji siku ya Ijumaa alizindua mchakato wa kukusanya angalau sahihi milioni kumi (10) ili kumbandua rais Ruto mamlakani.

 

 

 

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *