Ziara ya Rais Ruto Mlima Kenya yang’oa nanga Jumanne

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto aanza ziara ya siku tano Mlima Kenya.

Ziara ya Rais William Ruto katika eneo la Mlima Kenya imeng’oa nanga leo Jumanne, huku akitarajiwa kuzindua na kukagua miradi ya maendeleo.

Siku ya Jumanne kiongozi wa taifa anatarajiwa kuzuru maeneo ya Rumuruti, Nanyuki na Naromoru, akisema ziara hiyo inanuiwa kutoa maelezo ya kazi ya serikali ya Kenya Kwanza kwa wapiga kura wa eneo hilo.

Huku akianza ziara hiyo ya siku tano katika eneo hilo, Rais Ruto alipuuzilia mbali madai kwamba kuna uhasama kati yake na wakazi wa eneo hilo, akielezea imani yake katika uhusiano wake wa muda mrefu na wakazi wa Mlima Kenya.

“Mimi nimekuwa nikitembea Mlima Kenya kwa miaka 20, huu urafiki nimetengeneza na watu wa mlima Kenya hauwezi kupimwa kwa miezi michache,” alisema Rais Ruto alipokuwa akihojiwa na wanahabari katika ikulu ndogo ya Sagana, Jumatatu usiku.

Katika ziara yake, Rais Ruto anatarajiwa kuzindua miradi iliyokamilika, kukagua miradi inayoendelea, na kuzindua mipango mipya katika kaunti za Laikipia, Nyeri, Meru, Kirinyaga, Nyandarua, Murang’a, Embu, Tharaka-Nithi na Kiambu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *