Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfuta kazi kamanda mkuu wa jeshi la anga la Ukraine, Mykola Oleshchuk, tovuti ya rais imechapisha taarifa hiyo.
“Nikolai Nikolaevich Oleshchuk ameondolewa kwenye cheo cha Kamanda wa Jeshi la Anga la Jeshi la Ukraine,” inasema.
Zelensky pia alichapisha ujumbe wa video kuhusu taarifa hiyo.
“Nimeamua kubadilisha kamanda wa esjhi la anga la Ukraine. Ninashukuru sana marubani wetu wote wa kijeshi, wahandisi, askari wa kikundi cha wanajeshi wanaohama, wafanyikazi wa ulinzi anga. Kwa wote ambao kusema kweli hupigana kwa ajili ya Ukraine. Muwajali watu. Wajali wafanyakazi. Tuwatunze wanajeshi wetu wote,” alisema.
Luteni Jenerali Anatoly Krivonozhko, ambaye aliongoza kituo cha jeshi la anga la Ukraine, ameteuliwa kuwa kaimu kamanda wa leshi la anga.