Zari amtetea mume wake Shakib

Shakib amehusishwa kwenye msimu wa tatu wa kipindi Young, Famous & African cha Netflix na wengi wanatilia shaka uwezo wake wa kuzungumza kiingereza.

Marion Bosire
2 Min Read

Mfanyabiashara maarufu wa asili ya Uganda Zarina Hassan amemtetea mume wake Shakib, kufuatia matamshi yake ya lugha ya kiingereza.

Hii ni baada ya video ya kutangaza ujio wa msimu wa tatu wa kipindi cha Netflix ‘Young, Famous & African’ kuchapishwa mitandaoni.

Wengi wa waliotoa maoni yao kuhusu video hiyo, walitilia shaka uwezo wa Shakib wa kuwasiliana kwa kiingereza ikitizamiwa kwamba ameathirika zaidi na lafudhi ya kiganda.

Lakini Zari alimtetea kupitia video akisema hata kama ana lafudhi nzito ya Kiganda, ameafikia mengi maishani kama vile kuweza kumwoa na kuhusishwa katika kipindi anachokitaja kuwa jukwaa kubwa zaidi ulimwenguni.

Kulingana naye, huu ni msimu wa ushindi kwa mume wake ambaye anasema huenda hata akamzidi akaingia kwenye tasnia inayomezewa mate zaidi ulimwenguni ya burudani ulimwenguni Hollywood.

Zari alizungumzia pia hatua ya wengi kuanza kuridhia mume wake hata ingawa mwanzoni hawakuwa wanampenda. “Naonya nyote mnzaanza sasa kumpenda mume wangu na mlitudhihaki mwanzoni.” alisema Zari.

Msimu wa tatu wa kipindi hicho cha’Young, Famous & African’ utazinduliwa rasmi Januari 17 kwenye Netflix na unahusisha wahusika wapya.

Wahusika hao wapya wanajumuisha Shakib, mtengeneza maudhui ya mitindo ya mavazi na maisha wa Afrika Kusini Kefilwe Mabote na mwigizaji wa Nigeria Ini Edo.

Wahusika ambao wanarejea kwa mara nyingine ni Zari, Khanyi Mbau, Nadia Nakai, Annie Macaulay-Idibia, Luis Manana, Swanky Jerry, Naked DJ, Kayleigh Schwark na Diamond Platnumz.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *