Tume ya Uchaguzi nchini Zambia, imefutilia mbali shughuli ya kuhesabu kura kote nchini humo, ikitaja kushambuliwa kwa baadhi ya maafisa wa uchaguzi na wizi wa karatasi za kupigia kura.
Aidha,tume hiyo imesema itatafakari kuhusu uamuzi huo baada ya saa 24.
Kamishna Mkuu wa tume hiyo Brown Kasaro, alisema ghasia katika baadhi ya wilaya nchini humo, ziliwalenga maafisa wa uchaguzi.
“Ghasia hizo zinawalenga maafisa wa uchaguzi na wizi wa karatasi za kupiga kura,” alisema Kasaro.
Zambia ilishiriki Uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi, huku Rais Hakainde Hichilema ambaye ameongoza taifa hilo tangu mwaka 2021, akikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Brian mundubile mwenye umri wa miaka 55.
Mbali na kumchagua rais, wapiga kura zaidi ya milioni nane waliojiandikisha walipata fursa ya kuchagua bunge jipya na mabaraza ya serikali za mitaa.
Watu milioni 8.7, wamesajiliwa kuwa wapiga kura nchini humo.