Shule za Kakamega na Yala zatikiswa na Uganda

Kesho Jumamosi, kakamega itakabana koo na Urambo (TZ) sawa tano usubuhi, kisha Yala ichuane na Morogoro alasiri.

KBC Digital News
1 Min Read

Mabingwa mara 13 wa soka ya wavulana baina ya shule za upili nchini Kenya Kakamega na nambari mbili wa mwaka huu Yala,wameanza vibaya mawindo ya taji la Afrika Mashariki baina ya shule za upili baada ya kurambishwa sakafu na shule za nchi ya Uganda mjini Morogoro nchini Tanzania.

Kwenye ngarambe hizo za ufunguzi, Yala ilizamishwa bao moja kwa nunge nayo kakamega ambayo pia ni mabingwa wa mwaka huu, ikasakamwa mabao mawili kwa moja na Mabingwa mara 13 wa taji hilo  St.Mary’s Kitende na Kyandondo zote za Uganda mtawalia.

Kesho Jumamosi, kakamega itakabana koo na Urambo (TZ) sawa tano usubuhi, kisha Yala ichuane na Morogoro alasiri.

Share This Article