Zambia na Equitorial Guinea wakijikatia tiketi kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika.
Zambia walifuzu baada ya kuwazabua Ivory Coast mabao matatu kwa bila mjini Lusaka.
Equatorial Guinea pia wakifuzu kama viongozi wa kundi lao.
Katika matokeo mengine ya mechi hizo za raundi ya tano zilizopigwa Jumamosi, Afrika Kusini hatimaye iliwashinda Morocco mabao 2-1 baada ya subira ya miaka 21, huku mabingwa watetezi Senegal wakiambulia sare ya bao moja ugenini dhidi ya Benin.
Mataifa yaliyofuzu kwa kipute cha mwakani ni Afrika Kusini,Morocco,Zambia,Equatorial Guinea, Senegal,Burkina Faso, Tunisia, Algeria, Misri na wenyeji Ivory Coast.