Zambia kuanza ujenzi wa miundombinu ya umeme kuunganisha Tanzania

BBC
By
BBC
1 Min Read

Zambia itaanza tena ujenzi wa miundombinu ya umeme unaounganisha na Afrika Mashariki, na kuunda moja ya masoko makubwa ya nishati ulimwenguni, afisa mwandamizi wa Benki ya Dunia alisema Ijumaa.

Mradi huo wa umeme wa Zambia na Tanzania umepangwa kuanza tena mwezi huu, na kukadiriwa kukamilika mnamo mwaka 2028, Achim Fock, meneja wa nchi ya Zambia katika Benki ya Dunia, alisema Ijumaa wakati wa sherehe ya kutia saini.

Mradi wa dola 320,000,000 wa kuunganisha vifaa vya umeme vya Zambia na Tanzania unafadhiliwa na Benki ya Dunia, Jumuiya ya Ulaya na Uingereza.

Gharama ya kazi iliyosalia ni $ 298 milioni, ambayo ruzuku ya Benki ya Dunia itashughulikia dola milioni 245, Kaimu Waziri wa Fedha Chipoka Mulenga alisema, katika hafla hiyo hiyo.

Mradi huo ulianza kwa mara ya kwanza zaidi ya muongo mmoja uliopita lakini umesitishwa kwa sababu tofauti, hivi karibuni ikiwa ni kwa sababu ya COVID-19 na wasiwasi juu ya deni la Zambia mwishoni mwa 2020.

Fock alisema soko la pamoja lenye kuunganisha mabwawa ya umeme Kusini na Mashariki ya Afrika yatasaidia kupunguza gharama za umeme, kuongeza nishati na kuunda fursa mpya za kibiashara na uwekezaji katika sekta ya umeme kote Afrika.

BBC
+ posts
Share This Article