Zaidi ya watu 600 wafariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Morocco

Dismas Otuke
1 Min Read

Zaidi ya watu 600 wameaga dunia kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea  nchini Morocco .

Kulingana na maafisa wa usalama tetemeko hilo la ardhi lililokuwa la ukubwa wa ukubwa wa 6 nukta 8 katika vipimo vya richa limetokea majira ya saa saba usiku wa manane  kuamkia Jumamosi, katika eneo la milima ya Atlas kilomita 71 kutoka mjini Marrakesh na kuporomosha majengo kadhaa .

Walioshuhudia wamesema nguvu za umeme ,na mindatao ya simu ilitoweka kwa takriban dakika 10 wakati wa mkasa huo uliotokea katika maeneo ya Al-Haouz, Marrakesh, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant.

Hospitali nyingi eneo la Marrakesh limewaomba wananchi kufika hiospitalini ili kuchangia damu .

Eneo la kusini mwa Marrakesh ni maarufu sana kwa shughuli za kitalii na yamkini watu wengine 392 wamelazwa hospitalini kutokana na majeraha.

Kwa mjibu wa vyombo vya habari nchini Morocco  tetemeko hilo la ardhi ndilo kubwa na baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Website |  + posts
Share This Article