Zaidi ya washiriki 10,000 wamejisajili kushiriki makala ya 3 ya mbio za Nairobi City Marathon, zitakazoandaliwa Jumapili hii.
Kulingana na waandalizi washiriki 731 wakiwemo wa kigeni 40 wamejisajii kwa mbio za marathon,3,500 kwa mbio za kilomita 21 ,4,200 kwa kilomita 10 na 1,900 kwa mbio kilomita 6.
Idadi hiyo hata hivyo inatarajiwa kupanda hadi 15,000 kufikia siku ya mwisho ya usajili Jumamisi hii.
Kulingana na Mkurugenzi wa mbio hizo Ibrahim Hussen,wamepima barabara itakayutima kikamilifu, ili kuhakikisha wanatimiza vigezo vya shirika la kimataida la mbio za barabarani AIMS.
Barabara kuu za kutoka na kuingia katikati ya jiji zitafungwa baina ya Jumamosi saa sita usiku wa manane na Jumapili saa nane adhuhuri.
Lengo kuu la mbio hizo ni kutangaza jiji la Nairobi kuwa kivutio cha watalii, huku vitengo vyote vinne vikishuhudia washiriki wakikimbilia katika barabara ya Express Way.
Washindi wa Marathon watatuzwa shilingi milioni 3.5, nafasi ya pili milioni 2.2 na milioni 1.5 kwa watakaomaliza katika nafasi za tatu.
Washindi wa kilomita 21 watatuzwa shilingi laki moja unusu,nafasi ya pili 80,000 na 50,000 kwa watakaomaliza nafasi za tatu.
Washindi wa kilomita 10 watapokea shilingi laki moja, huku kukiwa na zawadi ya pesa jumla ya shilingi milioni 24.
Robert Kipkemboi na Naomi Jebet walitawazwa mabingwa wa marathon mwaka uliopita.