Wanafunzi zaidi ya 200 wanufaika kwa msaada wa masomo

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanafunzi 205 wamenufaika na msaada wa masomo ya vyuo wa kima cha shilingi milioni 12 kutoka kwa wakfu wa Prudence, unaomilikiwa na kampuni ya bima ya Prudence.

Msaada huo ulitolewa kwa hazina ya elimu nchini na utawafaidi wanafunzi wa masomo ya mwaka wa kwanza vyuoni kila mwaka, huku watakaonufaika wakiwa wale wanaotoka familia maskini kote nchini.

“Kila mwaka, zaidi ya wanafunzi laki mbilu hufuzu kujiunga na elimu ya vyuo lakini wengi wao ambao ni werevu hukosa kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa karo.”

Katika kampuni ya Prudence, tumetilia maanani swala hili na ndio maana tumeshirikiana na Wizara ya Elimu kuwapiga jeki wanafunzi,” alisema Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *