Wagonjwa zaidi ya 200 wa mtoto wa jicho wafanyiwa upasuaji bila malipo Turkana

Francis Ngala
3 Min Read
Madaktari wa macho kutoka hospitali ya Lion sightfirst, wakitoa huduma kwa wagonjwa.

Zaidi ya wagonjwa 200 wa mtoto wa jicho katika kaunti ya Turkana wamenufaika na huduma ya upasuaji wa bila malipo kutoka kwa hospitali ya Lion Sightfirst ambao walipiga kambi katika hospitali za katilu na Lokichar, Turkana kusini kutoa huduma ya afya ya bila malipo Kwa ushirikiano na wizara ya afya ya kaunti ya Turkana.

Kambi hiyo imevutia idadi kubwa ya wagonjwa kutoka maeneo Bunge tofauti katika kaunti ya Turkana ambapo waliofika kupata huduma walipimwa na kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataract.)

Kulingana na Leah Naukot mmoja wa wagonjwa walionufaika na zoezi hili la huduma ya afya bila malipo anasema kuwa kwa muda amekuwa akihangaika sana kutokana na kuumwa na macho.

“Niligongwa na mti nilipokua nikichoma makaa ili niuze nilishe watoto,sasa kutoka wakati huo wote nimekua nikisumbuliwa na macho sasa niliposikia kuna watu wamekuja kutusaidia nikaamua kuja ili nitibiwe sasa nashukuru sana hawa madaktari Sana Kwa msaada wao”,Leah Naukot alisema.

Mratibu wa maswala ya magonjwa ya macho katika kaunti ya Turkana Samson Akichem Lokele amesema kuwa wanalenga wagonjwa 1000 wa cataract kila mwaka na pia kutoa wito Kwa wahisani kujitokeza kupiga vita ugonjwa wa cataract katika kaunti ya Turkana.

“Kaunti ya Turkana iko katika asilimia 52 ambayo ni asilimia kubwa humu nchini,mpaka sasa tumetibu wagonjwa 200 wa cataract na pia tunalenga wagonjwa 1000 wa cataract mwaka ukiisha,na kama wizara ya Afya kaunti ya Turkana tutasaidiana na wahisani wote Kwa manufaa ya wakaazi wa kaunti ya Turkana”, Samson Akichem Lokele alisema.

Wataalam wa magonjwa ya macho kutoka hospitali ya lions sightfirst wamesema kuwa wao hutibu magonjwa ya cataract na matatizo yatokanayo na cataract na pia kuwafuatilia waliofanyiwa upasuaji, cataract inaweza kusababishia mtu kuwa kipofu usiposhughuliwa mapema.

Mtoto wa Jicho ni Nini ?

Mtoto wa jicho ni hali ya lenzi ya jicho kuwa na ukungu, ambayo husababisha kupungua kwa uwezo wa kuona na, kwa baadhi ya visa, upofu. Hali hii hutokea pale ambapo protini zinapojikusanya kwenye jicho moja au yote mawili, na kuzuia retina kufanya kazi vizuri.

Ugonjwa wa mtoto wa jicho kwa kawaida huathiri wazee, lakini unaweza kuwepo tangu utotoni, kusababishwa na mionzi au majeraha, pamoja na matatizo yanayotokana na upasuaji.

Mtoto wa jicho ni miongoni mwa sababu kuu za upofu duniani na ni mojawapo ya sababu za kawaida za kupoteza uwezo wa kuona kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 40.

Mtoto wa jicho unaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji, na hatua zinaweza kuchukuliwa ili kusaidia kuzuia kuanza kwa tatizo hili.

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *