Zaidi ya 50 wafariki kutokana na pombe mbaya India

Marion Bosire
1 Min Read

Watu zaidi ya 54 wameripotiwa kufariki baada ya kunywa pombe iliyokuwa na kemikali aina ya Methanol katika jimbo la kaskazini mwa India la Tamil Nadu.

Wengine wengi wamelazwa kwenye hospitali mbali mbali kwa sababu hiyo ambapo watu wapatao 200 wametibiwa tangu Jumatano katika wilaya ya Kallakurichi na wengine zaidi ya 100 bado wamelazwa.

Kati ya vifo vilivyoripotiwa, 48 ni wanaume na 6 ni wanawake na waathiriwa wote walikuwa wanalalamikia maumivu ya tumbo pamoja na dalili kama kutapika na kuhara.

Katika eneo hilo watu hununua pombe haramu kwa sababu ni wachache wanaweza kumudu gharama ya pombe halali. Wauzaji wa pombe hizo haramu huongeza Methanol kwenye pombe hizo ili kuongeza makali yake.

Kemikali ya methanol inafahamika kwa kuwa na sumu kali na mara nyingi hutumika viwandani. Ikiingia kwenye mwili wa binadamu inaweza kusababisha kupofuka, kuharibu ini na hata kifo.

Watu saba walikamatwa kuhusiana na pombe hiyo haramu huku lita zipatazo 200 zikitwaliwa.

Serikali ya jimbo la Tamil Nadu ilitangaza adhabu kali dhidi maafisa 10 waliojukumiwa kupambana na pombe haramu katika eneo husika kwa kukosa kuwajibika

Waathiriwa watapokea fidia kutoka kwa serikali huku uchunguzi ukianzisshwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *