YY Comedian atengana na mpenzi wake Noela Toywa

Alikuwa akihojiwa wakati alifichua utengano huo.

Marion Bosire
1 Min Read
YY Comedian

Mchekeshaji wa Kenya YY na mpenzi wake Noela Toywa wametangaza kwamba wametengana miezi miwili tu baada ya kutangaza uhusiano wao.

YY na Noela walionekana kama watu ambao walikuwa wanapendana sana kutokana na picha na video zao za pamoja lakini uhusiano wao umefikia kikomo.

YY alikuwa akihojiwa wakati alifichua hayo lakini hakutaka kutoa habari zaidi.

“Tulitengana kama vile watu hutengana. Ni maisha, sasa tuzungumzie onyesho langu.” alisema mchekeshaji huyo alipoulizwa kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi.

YY anaandaa tamasha la vichekesho katika ukumbi wa KICC Mei 25, 2025 kwa udhamini wa Access Light Media na kulingana na bango ni yeye pekee atatumbuiza siku hiyo.

Noela naye amechapisha kwenye Insta Stories picha inayoonekana kuwa kwenye studio fulani na jamaa mmoja na kuandika, “Kitu kinaandaliwa watu wangu. Kuwa tayari kusikia sauti yangu.”

Aliongeza kwamba kitu hicho kitajaa furaha na ujuzi na huenda ikawa pia yeye anaanzisha kipindi chake. Hajasema lolote kuhusu kutengana na YY.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *