Yul Edochie ajibu nduguye Lincoln kuhusu kuonyesha ndoa yake mitandaoni

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa Nollywood ambaye pia anahusika na uandaaji wa filamu Yul Edochie, amemjibu kakake mkubwa Lincoln Edochie aliyemshauri aache kuweka ndoa yake na mke wake wa pili mitandaoni.

Lincoln alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha mitandaoni cha mwigizaji nguli Kanayo O Kanayo ambapo alitakiwa kutoa maoni yake kuhusu ndoa ya Yul na mke wa pili Judy Austin.

Alijibu kwamba kama wanafamilia wangependelea Yul aache kuweka ndoa yake na Judy Austin mitandaoni kwani kuna wale ambao anadhalilisha kama vile mke wake wa kwanza may.

Kulingana naye, baba yao ambaye ni mwigizaji mkongwe wa Nollywood Pete Edochie huwa anawashauri wasiweke masuala ya ndoa na familia mitandaoni.

Yul kupitia Instagram alijibu hilo bila kutaja yeyote akisema kwamba wanaomshauri afiche ndoa yake ya pili na wajinga na kwamba hata wanaoficha huishia kwenye talaka.

“Kila mtu amegeuka kuwa mshauri mitandaoni. Maisha yenu yanasambaratika hamwezi kuyarekebisha. Lakini mnaweza kushauri watu wengine.” aliandika Yul.

Aliendelea kushangaa wanavyoathirika akichapisha picha na video za mke wake mitandaoni. “Ni nyinyi mnaninunulia deta au ni mke wenu ninachapisha?” alimalizia Yul.

Yul amekuwa akikashifiwa na wengi mitandaoni kufuatia hatua yake ya kuoa mke wa pili mwigizaji Judy Austin, huku mke wake wa kwanza May akionekana kukasirishwa na hatua hiyo.

Share This Article