Yul amwomboleza babake

Amemtaja marehemu Pete Edochie kuwa baba mwenye upendo, mfano bora wa kuigwa na mmoja wa watu wenye moyo mwema zaidi aliowahi kuwafahamu

Marion Bosire
1 Min Read
Pete Edochie na Yul Edochie

Mwigizaji wa Nigeria, Yul Edochie, amemwomboleza babake Pete Edochie ambaye pia ni mwigizaji mkongwe wa filamu za Nollywood aliyefariki kwa hisia kali.

Amemtaja kuwa baba mwenye upendo, mfano bora wa kuigwa na mmoja wa watu wenye moyo mwema zaidi aliowahi kuwafahamu.

Katika ujumbe wa kugusa moyo aliouchapisha kwenye Facebook, Yul alieleza masikitiko makubwa na kutokuamini kifo cha babake, akisema alitamani aendelee kuwa hai kwa miaka mingi zaidi.

Alikumbuka nyakati zao za pamoja, mazungumzo marefu, vicheko na mawasiliano ya kila siku. Alisema babake alitamani kuwa naye karibu muda wote na aliendelea kujali hali yake hadi dakika zake za mwisho.

Yul pia alikumbuka walipokutana hospitalini kwa mara ya mwisho, ambapo babake alimwomba amshike mkono.

Mwigizaji huyo alisifu urithi wa Pete, akimtaja kama mtu mwadilifu, mkarimu na mnyenyekevu ambaye aligusa maisha ya watu wengi barani Afrika na nje kupitia kazi yake ya uigizaji.

Alimshukuru Mungu kwa kumpa nafasi ya kuwa mwanawe, akisema anafurahi kuwa alimfanya ajivunie na kuendeleza urithi wa familia yao katika tasnia ya Nollywood.

Yul alihitimisha ujumbe wake kwa kumwomba babaake amwongoze mwanawe Kambi, ambaye anaamini huenda Pete tayari amekutana naye huko ahera.

Share This Article