Young Kings kutoka Dandora na Dagoretti Mixed Girls ndio mabingwa wa makala ya nne ya mashindano ya Safaricom Chapa Dimba eneo la Nairobi .
Young Kings walitoka nyuma bao moja na kuicharaza Dagoretti Lions mabao 6-1, katika fainali iliyopigwa katika uwanja wa Dandora siku ya Jumapili.
Katika fainali ya wasichana Dagoretti Mixed Girls walitawazwa mabingwa baada ya kuigaraggaza Misericordiae Queens ya Makadara magoli sita kwa bila .
Dandora Young Kings na Dagoretti Mixed Girls’ walituzwa shilingi 250,00 kila moja na tiketi ya kushiriki mashindano ya kitaifa kuwakilisha eneo la Nairobi ,wakati wa fainali za mwezi ujao katika kaunti ya Kisumu.