Xavier Nato ambaye ni mwandishi wa hati za maigizo, mwigizaji na mwelekezi wa maigizo amefariki.
Kifo chake kinajiri baada yake kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi ambao pia ulimsababishia matatizo ya figo.
Wakenya wengi wamemuomboleza kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakikosa kuamini kwamna ametoweka.
Mwigizaji Alvina Gachugu alioshangazwa na habari za kifo chake akisema Xavier alikuwa mmoja wa waelekezi wake wa kwanza alipoanza kuigiza.
“Nilikuwa na umri wa miaka 18 na nilimhoji kwenye runinga ya TVC ambapo nilikuwa mtangazaji mwanagenzi.” aliandika binti huyo chini ya video fupi aliyochapisha ya mahojiano hayo.
Mwezi Novemba mwaka huu wa 2024, familia yake iliomba usaidizi wa kifedha wa kugharamia matibabu yake.
Xavier aliyekuwa anamiliki kampuni ya uigizaji ya Millaz Productions alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda mrefu na matibabu yake yalikuwa ghali.