Wydad Casablanca waikalifisha Esperance mbele ya umma na kutinga fainali

Dismas Otuke
1 Min Read

Wydad Casablanca  wamestahimili shinikizo kali kutoka kwa wenyeji Esperance Sportive du Tunis, na kuwa timu ya kwanza kufuzu kwa fainali ya makala ya kwanza ya Ligi ya soka Afrika, AFL baada ya kupata ushindi wa penati 5-4 kufuatia sare ya goli 1 baada ya duru mbili za semi fainali.

Wydad waliocheza kwa tahadhari kubwa walilazimisha kipindi cha kwanza cha marudio ya nusu fainali uwanjani Rades, kuishia sare tasa  na kuwahini vijana wa nyumbani fursa ya moja kwa moja kupachika goli licha ya kumiliki mpira kwa kipindi kirefu.

Mshambulizi wa mzawa wa Brazil  Rodrigo Rodrigues, alipachika goli pekee kwa wenyeji kunako dakika ya 66 na kulamilisha pambano kumalizia sare baada ya Wyda pia kushinda duru ya kwanza bao moja kwa bila.

Kipa wa Wydad Youssef El Motie, alikuwa nyota wa mechi  baada ya kupangua penati ya mshambulizi  Rodrigues na kuwapaisha hadi fainali .

Mshindi wa kombe hilo atabugia shilingi milioni 600 za Kenya huku timu ya pili ikiondoka na burungoto la shilingi milioni 450,000.

Share This Article