Wydad Casablanca ya Morocco itawaalika Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mkondo wa kwanza wa fainali ya kombe la AFL Jumapili Novemba 5, kuanzia saa tatu usiku katika uwanja wa Mohammed V mjini Casablanca Morocco.
Mkondo wa pili utaandaliwa nchini Afrika Kusini huku timu mshindi ikitunukiwa shilingi milioni 600 za Kenya na milioni 450 kwa timu itakayomaliza nafasi ya pili.
Mashindano hayo ambayo ni ya makala ya kwanza yameshrikisha vlabu vinane bora barani Afrika, na yanafadhiliwa na Kinara wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Gianni Infantino.
Ili kutinga fainali Mamelodi iliwabandua washindi mara 11 wa ligi ya mabingwa Afrika ,Al Ahly ya Misri kwa ushindi wa bao 1 kwa nunge, nao Wydad Casablanca wakaitema nje Esperance ya Tunisia penati 5-4, kufuatia sare ya bao moja kutokana na mikumbo miwili.
Mikondo yote miwili ya fainali itarushwa mubashara kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1.