Wizara ya Utalii kushirikiana na vyombo vya habari kuinadi Kenya

Martin Mwanje
1 Min Read

Wizara ya Utalii na Wanyama Pori itashirikiana na vyombo vya habari kunadi mandhari ya kupendeza nchini, wanyama pori wa kipekee na turathi za kitamaduni ili kuinadia Kenya kwa dunia.   

Ushirikiano huo umeasisiwa wakati wa mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Utalii Peninah Malonza, wahariri na wanahabari kutoka vyombo vikuu vya habari nchini.

Chini ya ushirikiano huo, vyombo vya habari vitatarajiwa kuhamasisha na kuhifadhi utalii tunu wa nchi, wanyama pori na turaathi za kitaifa kupitia kuangazia vyote hivyo kwa njia chanya. Kwa Pamoja, vitatumia maazungumzo ya wazi na yenye tija kuchochea shabaha moja yaa kuinadi Kenya kwa dunia.

Malonza amesema vyombo vya habari viinatekeleza jukumu muhimu kama mshirika kuvizungumzia kwa njia huru vivutio mbalimbali vya utalii nchini.

“Kinachoifanya Kenya kuwa nchi ya kipekee duniani ni turathi zake za kitamaduni za kuvutia zilizosukwa kwa karne kadhaa pamoja na tamaduni na historia zinazotoa pumzi kwa roho ya nchi. Ufasaha wa vyombo vya habari wa kuzungumzia haya yote unatoa msisimko kwa watalii wa dunia wanaotamani kujionea na kutambua mengi,” alisema Malonza.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *