Wizara ya Utalii kuboresha mji wa Malindi

Marion Bosire
1 Min Read

Wizara ya Utalii imetangaza mpango wa kuboresha mji wa Malindi kwa lengo la kuvutia watalii zaidi.

Haya yaliafikiwa kwenye kikao cha kushirikisha umma kilichoongozwa na Waziri wa Utalii Dkt. Alfred Mutua aliyesema kwamba kazi itakayoanza mara moja ni ya kuweka taa za barabarani mjini Malindi.

Dkt. Mutua amesema mradi huo unafadhiliwa na serikali kuu kupitia kwa wizara yake.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wadau wa sekta ya utalii mjini Malindi wakiwemo wamiliki wa hoteli, wanaosafirisha watalii, wakazi wa eneo hilo na wawakilishi wa makundi ya kijamii.

Uboreshaji wa miundombinu katika mji huo ndio ulitajwa na washiriki wengi kama vile upanuzi wa uwanja wa ndege.

Usafi wa mji na fuo kwa jumla haukusazwa kwenye mazungumzo hayo, huku vyoo safi vikitajwa pia na serikali kuhimizwa kuboresha vilivyoko na kujenga vingine vingi katika maeneo tofauti ya mji huo.

Waziri Mutua aliombwa kuhakikisha kwamba umeme unakuwa wa kutegemewa mjini Malindi na barabara zinazoelekea kwenye fuo pia ziboreshwe.

Website |  + posts
Share This Article